Shida haipigi hodi, lakini hakuna shida isiyo na mwisho, wako wengi waliotangulia wamepata shida lakini shida zao zimebakia historia, wangine walitumia shida zao kuwa kisingizio cha kutorekea ngambo kwa kuteka ndege nyara kwa kutumia silaha za bandia lakini wakaishia kifungoni. Wengine walijaribu kuzamia meli na kuishia kutoswa baharini.Kufanya kazi kwa bidii ndiyo njia pekee ya kujiepusha na shida, tamaa ya kufika ngambo imeponza wengi. Wapo walioozea kifungoni, wapo waliokuwa chakula cha papa na wapo waliofanikiwa kufika ngambo lakini wanaishi na kulala mitaani na hawana namna yoyote ya kurudi nyumbani.
Veja mais